Monday, October 25, 2010

JIZI LAUMBUKA KWA KUSHINDWA KUBEBA MIHELA ALIYOIBA

Jizi moja jijini Sofia nchini Bulgaria lilifanikisha mpango wake wa wizi kwa kuiba fedha kibao mpaka akashindwa kuzibeba na hatimaye kutiwa nguvuni na Polisi wa jiji hilo kwa kushindwa kubeba furushi lake la pesa aliloliiba.

Jizi hilo liliiba sarafu zilizofikia dola za kimarekani milioni 9 na kuzibeba kwa kutumia usafiri wake wa pikipiki, usafiri huo ulizidiwa na uzito wa sarafu hizo na kusababisha kuanguka wakatika akijaribu kukimbia. Jamaa huyo mwizi aliumia vibaya na hatimaye alikamatwa na Polisi na kupelekwa sehemu husika kwa hatua zaidi.

2 comments:

  1. Si heri angegawia watu, ili apunguze mzigo, ...lakini wahenga husema za mwizi ni arubaini, au?

    ReplyDelete
  2. Arubaini zake zilikuwa zimetimia bila shaka!

    ReplyDelete