Sunday, October 31, 2010

MSAFIRI UNAJUA UNAPOENDA?

  
Jamaa akiwa safarini na mboga yake, nadhani huyo mboga aliyepewa msaada wa usafiri  angejua anapokwenda angeruka zake na kutoka nduki.

1 comment:

  1. Mhh! hiyo ndio siri ya sifuri, ukiweka namba mbele inapungua uzito na ukiweka nyuma ianongezeka thamani.
    Mlishe anenepe, upate kitoweo safi,...na hata kama yupo mzizini ambapo anajua kesho kwa yule kesho kwake, bado atarejea kwa bwana wake akilia meee, meee!
    Hiki ni kitendawili, cha mtoza ushuru, awapitia wenzake na kuwadai, lakini mwisho wa siku gharama yake inamwangukia hata yeye!
    Mwenye macho haambiwi tazama, ni hayo kwa mtizamo wa mbuzi juu ya bega la mpanda baiskeli!

    ReplyDelete