Saturday, October 9, 2010

SADAM HUSSENI ALIFIKISHWA KIZIMBANI KWA KESI 148 ZOTE ZA MAUAJI


Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti  alikuwa Rais wa Iraki, kunzia mwaka wa 1979 hadi  2003, pia alikuwa  waziri mkuu wa Iraki kati ya 1994 na 2003.
Alipanda ngazi ndani ya serikali na chama cha Baath kama makamu wa rais aliyemtangulia Ahmad Hasan al-Bakr. Baada ya kupewa cheo cha rais aliua wapinzani wengi ili kuimarisha utawala wake.
Akaanzisha vita mbili:
  • Vita kati ya Irak na Uajemi (1980 - 1988) aliyoanzisha baada ya kuona jeshi la Uajemi lilidhoofishwa kutokana na mapinduzi ya Ayatollah Khomeini; alishindwa kufikia shabaha zake akalazimishwa kukubali mkataba wa kusalimu amri na Uajemi.
  • Vita ya Ghuba ya 1990/91 alipoamuru jeshi la Iraki kuvamia nchi jirani ya Kuweit; hatua hii ilijibiwa na amri ya Umoja wa Mataifa Wairaki waondoke tena walipokataa jeshi la kimataifa lililoongozwa na Marekani lilifukuza Wairaki katika aridhi ya Kuweit.
Ndani ya Iraki alipigania upinzani wa sehemu kubwa za wananchi hasa katika kempeni dhidi ya Wakurdi katika kaskazini ya Iraki wakati wa vita dhidi ya Uajemi na dhidi Washia wa Iraki Kusini baada ya vita ya ghuba.
Saddam Hussein aliondolewa madarakani wakati wa uvamizi wa Iraki na Marekani katika vita ya pili ya ghuba mwaka 2003. Alienda mafichoni kwa miezi kadhaa akakamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama ya Kiiraki iliyompa hukumu ya mauti kwa jina dhidi ya binadamu na hasa kesi 148 za mauja zilizothibitishwa mahakamani.
Alihukumiwa kunyongwa Desemba 2006 katika kambi la kijeshi mjini Al Kadhimiya nchini Iraki.

1 comment:

  1. Moja kanuni inayoshindikana kuzungumziwa ni nini TAFSIRI YA UHALIFU WA KIVITA. kuna mengi ya kuongelea zaidi suala la Saddam Hussein kuliko tu kukubaliana na Joji Kichaka a.k.a Joji Bushi. Mara nyingi nimegomba kwamba UHALIFU WA KIVITA ni fasiri pana na kwa kuwa mataifa machanga na yale yasiyofuata itikadi ya bwana mkubwa yanachukuliwa kwa mantiki iliyopinda kwamba ni wahaini.

    wakubwa wanataka hawa wachanga wapige magoti na kuwalamba viatu, aghalabu nao wangelikuwa wakifanya hivyo tungelijua sote wanajua mantiki ya kujiamulia. kesi ya Charles Taylor pamoja na uhalifu wake lakini namna ushahidi unavyokusanywa kwa umbeya na ushangingi inashangaza kuona watu wanaojiita magwiji wa sheria wanakuwa vihiyo wa sheria za mahakama. Suala la UHALIFU WA KIVITA ni mantiki pinda sana, maana Tony Blair katika kitabu chake cha THE JOURNEY anaonekana kutubu kwa suala hilohilo. sasa sijui mantiki yake iko wapi hapa. je UHALIFU WA KIVITA UNAWAFAA KAINA MUGABE TU?

    ReplyDelete