Sunday, November 28, 2010

MFAHAMU MUAMMAR AL GADDAFI KIONGOZI WA LIBYA


Amiri Muammar al-Gaddafi ni kiongozi wa kiistori wa taifa la Libya. Kiongozi huyu miaka ya karibuni amejijengea heshima kubwa barani Afrika na katika Jumuia ya kimataifa kutokana na msimamo wake wa kutaka kuliunganisha bara la Afrika kuwa nchi moja.
Amezaliwa katika familia ya mabedawi (wafugaji wahamiaji) mnamo mwaka 1942. Baada ya masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Libya alijiunga na jeshi 1963 akasoma kwenye chuo cha kijeshi cha Sandhurst (Uingereza) 1965.
1 Septemba 1969 pamoja na maafisa wenzake alipindua serikali ya mfalme Idris I na kutangaza Jamhuri ya Kiarabu ya Libya.
Ingawa hana cheo rasmi anaendelea kutawala nchi yake akiitwa "Kiongozi wa mapinduzi ya 1 Septemba ya Jamahiriya ya Ujamaa ya watu ya Kilibya-Kiarabu".

No comments:

Post a Comment