Monday, November 29, 2010

SIKIA HII YA JIJI LA LONDON


Jamaa mmoja aliyekuwa bingwa wa kula katika migahawa tofauti katika jiji la London nchini Uingereza  kisha kuingia mitini bila kulipa, ametiwa mikono mwa vyombo vya dola vya jiji hilo baada ya kuwekewa mtego kwa muda mrefu.

Jamaa huyo alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kula bila kulipa katika migahawa mikubwa zaidi ya mitatu ya jiji hilo, miongoni mwa migahawa iliyokumbwa na mkasa huo ni Glass House na Connaught.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 27 amejitete kwa kudai kwamba hana kazi yoyote ya kuweza kumpatia kipato na jamaa zake wa karibu wamekataa kumpatia huduma ya chakula ndio maana ameamua kula katika migahawa mikubwa mikubwa na kisha kuingia mitini kiujanja ujanja.

No comments:

Post a Comment