Saturday, November 20, 2010

PAKA NA MAAJABU YAKE

Pamoja na mnyama paka kuhusishwa na mambo mengi ya kidunia hasa katika imani za kishirikia na mpaka kuna watu wanaamini kuwa mnyama huyu ana roho saba, yaani ni mgumu kufa na  hata ukitaka kukatisha maisha yake utalazimika kutumia nguvu za ziada, lakini hayo ni maneno tu ya binadamu na waswahili wanaseme penye wengi pana mengi.

Ila jambo moja la uhakika ambalo linaweza kuwa la ajabu kwa myama huyu ni uwezo wa kipekee wa kuona usiku kuliko binadamu. Inasemekana katika macho ya paka kuna Glass maalum yenye uwezo wa kukata mwanga na kutoa mwanga, pia inasemekana mnyama huyu anauwezo wa kuona vizuri nyakati za usiku  mara sita zaidi ya binadamu.

No comments:

Post a Comment