Tuesday, November 16, 2010

POLISI ABAMBWA NA SHAHADA

Asakari Polisi mmoja wa kike mwenye cheo cha sajini mkoani Kirimanjaro amefukuzwa kazi baada ya kupatikana na tuhuma ya kukutwa na shahada sita za kupigia kura, siku chahe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu. 

Askari huyo aitwaye Mary Stella Soko umri miaka 46 alifukuzwa kazi baada ya kutiwa hatiani katika mahakama ya kijeshi, hata hivyo katika utetezi wake alidai kuwa shahada hizi ni za ndugu za watuhumiwa ambao walizitumia kwa ajili ya kudhamini na baadae kuzitelekeza kituo cha Polisi.

Pamoja na kujitetea kwake huko hakuweza kuishawishi mahakama kuacha kumtia hatiani, kwa vile alishindwa kutoa utetezi wa kueleweka kwa nini shahada hizo zisihifawe kituoni badala ya kutembea nazo katika pochi yake. Kukamatwa kwa askari huyo kunatokana na polisi kupata taarifa zake toka kwa raia wema. Siku za karibuni kumekuwa na tetesi kuwa baadhi ya askari polisi wamekuwa wakijihusisha na vyama vya kisiasa.

No comments:

Post a Comment