Sunday, November 7, 2010

TANZANIA YENYE AMANI INAWEZEKANA

Baada ya madongo ya hapa na pale toka wa viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa katika kampeni na wakati wa uchaguzi, sasa mambo yameisha  watanzania tuunganishe nguvu zetu kujenga taifa lenye uchumi imara na amani ya kudumu, katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni za udiwani, ubunge na urais watanzania walikuwa katika makundi tofauti kulingana na tofauti ya itikadi na sera za vyama vyao na aina ya viongozi waliokuwa wanawataka kwa ajili ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa kuwa viongozi waliotakiwa na watanzania kuanzia udiwani, ubunge na urais wameshapatikana basi hatunabudi kuwaunga mkono na kushirikiana nao kujenga taifa letu hadi hapo utakapofika wakati wa uchaguzi ujao ndio tutaangalia tumekosea wapi na tumepatia wapi na kisha kufanya marekebisho ya viongozi hao tuliowachagua. Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza watanzania kwa uelewa na uvumilivu katika kipindi chote cha kampeni na wakati wa uchaguzi pia nawakumbusha amani iliyopo inapaswa kulindwa na kila mmoja wetu ili kuleta maendeleo kwani kukosekana kwa amani ni kukosekana kwa maendeleo. Kweli Tanzania yenye amani inawezekana.

2 comments:

  1. Ni kweli sasa ni nguvu za kitaifa, na ningefurahii kwamba, kila mkutanaoo anaoshiriki raisi `uchama' usionekane, labda uwe mkutano rasmi wa chama, ili kuondoa `wangu' au changu. sasa hivi ni sisi kama taifa!

    ReplyDelete
  2. Mkubwa na mimi nakuunga mkono kwa asilimia zote kwa sasa utaifa mbele chama baadae!

    ReplyDelete