Sunday, December 5, 2010

JELA KUJENGEWA FUKWE MAALUMU

Gereza moja kubwa na maarufu nchini Urusi lina mapango wa kujenga fukwe maalumu kwa ajili ya kupumzikia wafungwa, viongozi wa gereza hilo maalumu kwa watu watukutu wamesema wanakusudia kujenga fukwe hiyo maalumu kwa ajili ya kupumzikia wafungwa.

Pamoja na ujenzi wa fukwe hiyo maalumu pia inakusudiwa kuwekwa huduma ya kuchuliwa (massage) na vitanda maalumu vya kupumzikia juani kama zilivyo fukwe nyingine kubwa na maarufu. Iwapo mipango hivyo itakamilika huduma hiyo itatolewa mara moja kwa wiki ikiwa na lengo la kuimarisha Afya za wafungwa ambao asilimia kubwa wamekuwa katika gereza hilo kwa miaka mingi na wengine kupoteza maisha kutokana na kutofanya mazoezi.

No comments:

Post a Comment