Wednesday, December 8, 2010

USAFIRI WA MAHARUSI

Usafiri wa pikipiki maarufu kwa bodaboda umekuwa kwa kasi sana nchini na barani Afrika kwa miaka ya hivi karibuni.Pichani ni bibi na  bwana harusi wakiwa katika usafiri wa pikipiki (bodaboda) mara baada ya kufunga pingu za maisha.

3 comments:

  1. Basi kuna kisa kimoja kama hicho, bwana kaoa, na usafiri ni bodaboda, best wa bwana harusi akampenda binti harusi, na binti kumbe naye alishampenda, lakini huyu best hakuwa kajiweka wazi. Katika pilikapilika hizi za kupeleka mahari, nini na nini, huyu best akakutana na huyu binti harusi, best ikabidi aliweke wazi penzi lake kwa huyu binti, kuwa mimi nilishakupenda siku nyingi, lakini nilikuwa sijapata muda wa kukuambia, na jamaa yangu huyu kakuwahi, sasa naumia, ifanyeje.
    Wakapanga kuwa watoroke, kabla ya ndoa. Basi kwa aili ya kubana matumizi, ilikodiwa pikipiki moja kuwabeba binti na bwana harusi na best wake. Na kwa vile ndoa haijafungwa, ikapangwa best akae kati binti mbele kama picha ianvyoonyesha na bwana harusi nyuma. Wakamuomba wakamtonywa muendesha pikipiki kuwa wakifika kilimanai awe kama anaibinua, na huyu best atatumia mbinu za kumsukuma nyuma bwana harusu na ataanguka wao na mwendesha pikipiki watajifanya hawajui bomba hadi mji wa piki na siku ya pili yakw wanaingia Dar na kufunga ndoa ya wapendanao!
    Ikafanyika hivyo...hutaamini jamaa anatesa na kimwana wake hapa Dar, na wamebarikiwa mtoto mmoja, mwenzao mapaka leo analalamika aliyofanyiwa kijijini na kudai hatakodi tena bodaboda!

    ReplyDelete
  2. Hii iko poa sanaaa tena haina gharama sana.

    ReplyDelete