Saturday, December 4, 2010

TIGER WOODS WANAMICHEZO TAJIRI ZAIDI DUNIANI

Mcheza gofu maalufu duniani Tiger Woods toka nchini Marekani alizaliwa mwaka 1975 na jina lake halisi ni  Eldrick Tount inasemekana ndio mwanamichezo bora kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni na utajiri wake unafikia dola milioni 500. Mwanamichezo huyo mpenda vimwana anapata mshahara wa dola milioni 85 kwa mwaka. Inasemekana kuna uwezekano mkubwa akawa mwanamichezo wa kwanza kuwa bilionea

Mwanamichezo huyo anayemiliki boti yenye thamani ya dola milioni 20, magari ya kifahari yasiyo na idadi kamili na majumba matatu ya kifahari, pia Woods ana mikataba na makampuni makubwa ya vifaa vya michezo kama vile Nike na Titleist ambazo zinamuingizia dola milioni 60 kwa mwaka.

Kutokana na kipato chake kwa mwaka kuwa kikubwa ukilinganisha na wanamichezo wengine duniani, jarida la Forbes lilimtaja kuwa ni mwanamichezo tajiri zaidi duniani

No comments:

Post a Comment