Watoto mapacha Consolata na Maria ambao walizaliwa mwaka 1996 wakiwa wameungana katika Hospitali ya Ikonda wilayani Makete mkoani Iringa wamefanikiwa kufaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2010. Watoto hao yatima wanaolelewa na msamaria mwema baada ya wazazi wao kufariki walifaulu kwa kila mmoja kupata alama 151 ila wakipishana katika ufaulu wa kila somo jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa hawakutizamiana na wala hawakusaidiana wakati wa mtihani wao.
Watoto hao mapacha wanaosoma katika shule ya msingi Ikonda mkoani Iringa wamekuwa na bahati ya kuwa na marafiki wengi kutokana na tabia yao ya adabu, upendo na kujituma wawapo darasani.
hakika Mungu ni muweza!
ReplyDeletetunaimani Mungu atawaongoza vizuri watoto hao.
ReplyDelete