Friday, December 10, 2010

WEZI WAENDA NA WAKATI

Kuna kundi la wezi nchini Uingereza limebuni njia mpya ya wizi kwa kusaka mali za kuiba kupitia mtandao maarufu wa Google Earth. Mtandao wa Google Earth wenye uwezo wa kuonyesha miji na mitaa yoyote duniani sasa unatumiwa na wajanja kwa ajili ya kuangalia mali ya kuiba.

Pamoja na madhumuni ya mtandao huo ya kurahisisha mawasiliano ulimwenguni kuna wajanja wanaotumia mtandao huo vibaya kwa kufanya uhalifu. Maeneo makubwa yaliyokubwa na balaa hilo ni maeneo ya makanisa, kwani inasemekana kuna kesi za wizi toka  katika makanisa 8,000 toka sehemu mbali mbali za dunia.

Wezi hao kwa kutumia mtandao huo uangalia makanisa yaliyojengwa kwa madini yenye thamani kubwa ya aina ya lead, ambayo utumika katika ujenzi wa mapaa kisha uendelea na shughuli zao za kihalifu baada ya kuona kupitia mtandao wa Google Earth. Ama kweli mijizi ya ulaya inaenda na wakati.

No comments:

Post a Comment