Sunday, February 6, 2011

NI KWELI MITANDAO YA KIJAMII NI CHACHU YA NGONO?

Kukua kwa sekta ya mawasiliano duniani hasa ya simu, kupitia ujumbe mfupi wa maandishi  katika simu yaani (sms) na intanet na kupitia mitandao ya kijamii kama vile Tagged, Twitter na Facebook imeelezwa kwamba ni chachu ya ngono zembe kwa watumiaji wake.

Hayo yamebainika baada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa na Jarida la Men's Fitness la nchini Marekani. Inasemekana kabla ya kuanza kwa mitandao hiyo ya kijamii watu walichukua muda mrefu kukubaliana mpaka kufikia hatua ya kufanya ngono tofauti na sasa baada ya kuanza mitandao hiyo watu wengi wamejikuta wakiingiza kwenye mahusiano kwa muda mfupi. Utafiti huo pia unaonyesha wanaume wengi wanapenda kuandika kwenye mitandao ya intanet na wanawake wengi wanapenda kuandika ujumbe mfupi wa simu (sms).

Je utafiti huu una ukweli wowote? kama unadhani unafahamu lolote juu ya matumizi mabaya ya mitandao  hiyo uwanja ni wako tupashe.

2 comments:

  1. Kila kitu kinauzuri wake na ubaya wake, kwa aliyegundua alijua karahisha maisha ya wenzake, ili wawasiliane kwa haraka hasa wakati wa shida, lakini binadamu...mtundu akaona hapo ndipo pa kumpatia mke wa mtu, ufisadi na mazambi kibaoooh.

    ReplyDelete
  2. HILO ULILOSEMA NDIVYO LILIVYO. NINAZIDI KUSHUHUDIA WATU WANAVYOPIGIANA CM SANA KISA ALIMUONA KTK MITANDAO YA KIJAMII NA MAWASILIANO YANAPATIKANA HAPO HAPO. MPAKA WENGINE WAMEDIRIKI KUTAFUTA WATU WATAKAOTOKA NAO VALENTINE DAY KUPITIA MITANDAO HIII HII YA KIJAMII. NA UKIFUATILIA MWISHO WA URAFIKI HUO KATI YA KE NA ME HUISHIA KWENYE MAHUSIANO AMBAYO PIA MWISHOWE HUWA KILIO NA MAJUTO SABABU IKIWA TUNA KURUPUKIA WATU.

    ReplyDelete