Tuesday, August 30, 2011

TABIA HII HADI LINI?

Tabia ya kujichukulia sheria mkononi imekuwa ni tatizo kubwa nchini na ni kinyume na haki za binadamu. Hebu tazama picha hii wananchi wakijichukulia sheria mkononi kwa mtu anayedhaniwa kuwa ni mwizi, Je! mtu akiamua kumpakazia mtu kumwita mwizi kwa sababu zake binafsi na watu wakachukua hatua kama hii kwa mtu asiyekuwa na hatia? toa maoni yako jinsi gani tunaweza kukomesha hii tabia.

Saturday, August 13, 2011

AJALI BADO TATIZO KWETU

Ajali bado ni tatizo nchini kwani imekuwa ikikatisha maisha ya watanzania kwa wingi, je tatizo hili litaisha lini?

Sunday, August 7, 2011

SHERIA MKONONI

Tatizo la wananchi kujichukulia sheria mkoni kutokana na makosa yanayojitokeza katika jamii sio tatizo la nchini kwetu pekee, kama picha inavyoonyesha nchini India wananchi wamejichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto watu.

Tuesday, August 2, 2011

UNAKUMBUKA HII?

Unakumbuka hii? Enzi hizo muziki wa bongo umeshika kasi na kuheshimika mambo yalikuwa kama unavyoona pichani, bendi zetu maarufu ziliweza kumiliki mabasi makubwa kama haya, siku hizi bendi zetu badala ya kusonga mbele hatua tano zenyewe zinarudi nyuma hatua kumi.

Monday, August 1, 2011

RAMADHAN KAREEM

Blog hii inawatakia waislam wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Friday, July 22, 2011

TAARIFA KWA WADAU WA BLOG HII

Kwa kipindi cha mwezi mzima blog hii imekuwa haipo hewani kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu wadau wetu kuwa blog hii itaendelea kuwa up date kama kawaida kuanzia tarehe 01 Agost 2011.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Wednesday, June 22, 2011

WAKULIMA

Rais wa Tanzania Dr Jakaya M. Kikwete akiwa na wazazi wa Mh Pinda (waziri mkuu) maarufu kama mtoto wa mkulima.

Monday, June 13, 2011

JIFUNZE HII

Kuna umuhimu wa kila mmoja wetu kujifunza lugha hii ya watu wenye ulemavu wa masikio (viziwi) ili kurahisisha mawasiliano na watu wenye matatizo ya kusikia.

Sunday, May 29, 2011

HII ITAISHA LINI?

Hii itaisha lini? viumbe hawa wataacha lini kupata misukosuko hii ambayo usababisha ulemavu mpaka kifo. 
Hebu tufikirie njia sahihi ya kuwasaidia viumbe hawa.

Wednesday, May 25, 2011

TANZANIA BLOG AWARD - MUDA WA KUPENDEKEZA BLOG UMESOGEZWA MBELE

Muda wa kupendekeza majina ya blog zitakazoshiriki katika mashindano umesogezwa mbele. Hivyo tarehe ya kutuma majina ya blog hizo umebadilishwa kutoka tarehe 31 May 2011 kwenda tarehe 10 June 2011. Taarifa hii kwa mujibu wa waandaaji wa shindano.

Blog hii inakuomba msomaji popote ulipo usisahau kuipendekeza kushiriki shindano hilo kubwa na la kwanza hapa nchini.

INAKUWA AJE UNAAMKA UNAKUTA ZIGO KAMA HILI

Inakuwa aje asubuhi unaamka unakutana na zigo kama hili nyumbani kwako, kama wewe utafanya nini kwa haraka haraka?

Wednesday, May 18, 2011

MJI WA MOSHI KIBOKO KWA USAFI

Mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro ni mji unaovutia na unaoongoza kwa usafi nchini Tanzania na Afrika mashariki na kati. Mji huu umeweza kuwa msafi kutokana na manispaa ya mji huo kutunga sheria ndogo ndogo za kusimamia usafi katika mji huo, je! jiji la Dar es salaam linangoja nini kuiga mfano wa Moshi?

Tuesday, May 17, 2011

MWALIMU ABUNI ADHABU MBADALA

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi huko Nepal amebuni adhabu mbadala kwa watoto watukutu, badala ya kuwacha ama kuwapa adhabu nyingine stahili, yeye alibuni adhabu ya aina yake kama unavyoona pichani wanafunzi wanalala alafu yeye anatekeleza adhabu yake kwa kuwakanyaga vidole vya mkononi kwa kutumia pikipiki. Vipi watu wa haki za watoto duniani wanatuambia nini kuhusiana na adhabu kama hii kwa watoto wadogo kama hawa?

Saturday, May 14, 2011

DAR YETU HII

Dar es salaam jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania na moja ya majiji maarufu katika ukanda wa Afrika ya mashatiki na kati linazidi kupendeza.

Thursday, May 12, 2011

KOMANDOO KUVAA VIATU VYA OSAMA


Unajua kwamba  kundi la kigaidi  la Al  Qaeda lina mpango wa kumkabidhi Ilyas Kashmiri ambaye alikuwa ni Komandoo wa jeshi la Pakisatani, kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo kumrithi Osama Bin Laden aliyeuwawa na majeshi ya Marekani hivi karibuni.. Habari za ndani toka FBI nchini Marekani zinaelea kuwa Kashmiri ni gaidi mwenye nguvu kubwa na ushawishi katika matukio ya maangamizi.

Ilyas Kashmiri alikuwa mmojawapo wa makamanda waliopigana vita  kati ya Afghanistani na Urusi mwaka 1980 na inasemekana alipoteza kidole na jicho moja wakati wa vita hivyo.

Monday, May 9, 2011

HII NAYO KALI

Familia moja huko nchini Thailand inajihusisha na ufugaji wa nyoka aina ya Chatu, aina hii ya nyoka ni moja ya aina ya nyoka hatari waliopo duniani kwani wana uwezo wa kumeza wanyama kama mbuzi, mbwa na hata binadamu, hebu angalia picha hii mama na wanawe wakicheza na nyoka huyo hatari wanayemfuga. We unaiona aje hii?

Sunday, May 8, 2011

HAPPY MOTHERS DAY

Siku ya tarehe 08 Mei huwa ni siku ya kuwakumbuka mama zetu popote pale walipo duniani, ni siku ya kusema asante kwa malezi mazuri toka kwa mama zetu na siku ya kushukuru kwa kutuleta hapa dunia na pia ni siku pekee ya kumueleza ukweli mama na hata kumuomba msamaha kwa jambo ambalo unahisi halikumpendeza mama. Mimi nasema nakupenda mama M/mungu aimweke roho yako mahali peka peponi amin. R.I.P mama!

Tuesday, May 3, 2011

HUKO WHITE HOUSE MAMBO YALIKUWA HIVI

Wakati kikosi maaluma cha jeshi la Marekani cha Navy SEAL ambacho kina sifa ya kipekee duniani kutoka na kuwa na mafunzo ya aina yake ya kupambana baharini, nchi kavu na angani kikiwa kinapambana na wafuasi wa Osama Bin Laden kwa muda wa dakika 45 hali ilikuwa hivi katika Ikulu ya Marekani katika chumba maalum cha kutolea amri za mapigano wakifatilia kila kilichokuwa kinaendelea katika mapigano hayo ambayo yalisanabisha helkopta moja ya Marekani kulipuka angani. Pichani Rais mwa Marekani Barak Obama akiwa na maofisa wengine wa serikali na baraza la usalama wa taifa la nchi hiyo wakifatilia kwa makinini kinachendelea katika uwanja wa mapambano huko Pakistani.

Sunday, May 1, 2011

Osama bin Laden is dead

Osama bin Laden is dead, and the United States is in possession of his body, President Barack Obama is expected to announce shortly. Bin Laden's death is the result of some as yet unspecified U.S. action, Obama will announce, according to CNN and NBC News. Obama is due to address the nation at approximately 11pm from the White House.

USALAMA KWANZA

Usalama Kwanza: Jamaa ameamua kuweka ulinzi wa simu yake kwa mtindo wa aina yake. Msomaji unaiona aje hii?

Thursday, April 28, 2011

MAJIBU YA CHEMSHA BONGO

Chemsha bongo yetu katika post iliyopita imepata watu watano waliochangia kujibu na wote wamepatia kuwa yule waliyemtaja katika picha ndio jibu sahihi kabisa. Hakuna sababu ya kutaja kwa kuwa wote waliotaja jina walipatia kwa usahihi mkubwa.

Hongereni Sana!!

Tuesday, April 26, 2011

Saturday, April 23, 2011

SIKUKUU NYINGI HALAFU HAKIELEWEKI

Kwa mtaji huu na mambo kama haya nilazima tupige kambi katika ATM kama huyu mwenzetu.

Wednesday, April 20, 2011

KIKOMBE CHA BABU

Kikombe cha babu mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika kijiji cha Sumange huko Loliondo mkoani Arusha sasa kimeshika kasi baada ya watu toka nje ya nchi na watanzania wenye asili ya kiasia nao kuona umuhimu wake na kujikusanya kwenda kujisalimisha kwa babu. Je kweli kikombe cha babu kinatibu? kama kuna mtu aliyetayari kutoa ushuhuda wake baada ya kupata tiba ya kikombe cha babu na kupona ama kutopona  awasiliane na blog hii.