Mtoto wa kibongo anapata tabu kupata elimu japo tunaambiwa elimu yenyewe ndio elimu ya kiwango cha chini katika nchi za Afrika Mashariki. Hebu tazama aina ya mazingira ya kupata elimu na unategemea matokeo gani hapa? Watanzania tuamke kuchangia kutengeneza mazingira bora ya kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania.
Sunday, April 17, 2011
Thursday, April 14, 2011
PEMPAS ZA KWETU
Na watoto wetu uswazi nao wanavaa pempas pia, sio wenu pekee.Hebu angalia ubunifu wa wabongo, kila kitu kinawezekana "wao waweze wana nini sisi tushindwe tuna nini".
Tuesday, April 12, 2011
UNAKUMBUKA USAFIRI HUU?
Usafiri huu ulikuwa enzi zetu zileee, unaweka foleni ya kupanda basi wakati basi lenyewe bado halijafika kituoni na halijulikani litafika muda gani. Vituo vingine vilikuwa na ratiba ya basi ikionyesha muda kufika na kuondoka kituoni, hapo usafiri ulikuwa mabasi ya UDA na KAMATA, Unakumbuka usafiri huu?
Wednesday, April 6, 2011
MWANAMKE NA YANAYOMSIBU
Wakati dunia hivi karibuni imetoka kusheherekea siku ya mwanamke katika dunia yetu ikiwa ni pamoja na kukumbushana haki za msingi za mwanamke wa dunia ya sasa, bado mwanamke anaendelea kupata kipigo toka kwa mwanaume na kuonekana kama ni haki yake ya msingi. Tuungane kutokomeza unyama huu kwa mama na dada zetu kote ulimwenguni.
Tuesday, April 5, 2011
HUYU NDIO MWANAFUNZI WA KITANZANIA
Huyu ndio mwanafunzi wa kitanzania: Mwanafunzi huyu licha ya kupata elimu isiyo ya kiwango cha juu bado anapata shida kubwa kuifikia hiyo elimu.Ebu tazama mtoto wa kitanzania akipata shida kuifikia elimu, tufanye nini ili kumsaidia mtoto wa kitanzania katika tatizo hili sugu la usafiri waendapo na watokapo mashuleni?
Saturday, April 2, 2011
SOKA INA WENYEWE
Kweli soka ina wenyewe, hebu angalia picha hii hapa alafu pata picha ndo wazee wetu wa kibongo ndio wawe wanasakata soka, hali inakuwa aje hapo uwanjani?
Thursday, March 31, 2011
HESHIMA KWA MWANAMKE
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKEWA WANAUME
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape
heshima zao wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!
Tuesday, March 22, 2011
MWANZA MPYA
Mwanza Mpya: huu ndio muonekano wa jiji la Mwanza nchini Tanzania kwa sasa baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa wa barabara na baadhi ya majengo.
Monday, March 7, 2011
HAPA NDIO MAMBO YOTE
Hapa ndio mambo yote, kuna wengine wanasikia tu kuwa tuna mgao wa umeme kwa kuwa kina cha maji kimepungua katika bwawa linalotumika kufufua umeme la Mtera, hapa ndio Mtera penyewe.
Friday, February 11, 2011
RATIBA YA OFISI HII VIPI
RATIBA YA OFISI HII VIPI: Jaribu kuangalia kwa umakini ratiba hii ya ofisi, alafu toa maoni yako kama unaona kweli ratiba hii inafaa ama kutofaa kufatwa katika maofisi yetu.
CHEMSHA BONGO
Picha ya chini iliyokuwa Chemsha bongo ni picha ya jiji la Arusha. Kweli kuna mdau mmoja alichemsha bongo yake vizuri na kupatia. Bahati mbaya mdau huyo akupenda kuweka wazi jina lake, hongera sana mdau kwa kuchemsha bongo yako na kuwa sahihi. Kweli picha hiyo ni Arusha.
Tuesday, February 8, 2011
CHEMSHA BONGO YAKO HAPA
Picha hii ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Je! ni wapi hapa? Chemsha bongo yako kidogo.
Sunday, February 6, 2011
NI KWELI MITANDAO YA KIJAMII NI CHACHU YA NGONO?
Kukua kwa sekta ya mawasiliano duniani hasa ya simu, kupitia ujumbe mfupi wa maandishi katika simu yaani (sms) na intanet na kupitia mitandao ya kijamii kama vile Tagged, Twitter na Facebook imeelezwa kwamba ni chachu ya ngono zembe kwa watumiaji wake.
Hayo yamebainika baada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa na Jarida la Men's Fitness la nchini Marekani. Inasemekana kabla ya kuanza kwa mitandao hiyo ya kijamii watu walichukua muda mrefu kukubaliana mpaka kufikia hatua ya kufanya ngono tofauti na sasa baada ya kuanza mitandao hiyo watu wengi wamejikuta wakiingiza kwenye mahusiano kwa muda mfupi. Utafiti huo pia unaonyesha wanaume wengi wanapenda kuandika kwenye mitandao ya intanet na wanawake wengi wanapenda kuandika ujumbe mfupi wa simu (sms).
Je utafiti huu una ukweli wowote? kama unadhani unafahamu lolote juu ya matumizi mabaya ya mitandao hiyo uwanja ni wako tupashe.
Wednesday, February 2, 2011
MISRI AMANI INAANZA KUTOWEKA
Amani ya Taifa la Misri inaanza kutoweka taratibu baada ya wananchi wanaopiga serikali ya nchi hiyo kuanza kupambana na watu wanaounga mkono serikali hiyo. Hii ni dalili mbaya kwa taifa hili ambalo ni moja ya mataifa yenye nguvu kiuchumi barani Afrika.
Friday, January 28, 2011
Tuesday, January 25, 2011
HII NAYO VIPI?
Mabango mengi ya matangazo tena yenye muonekano bora yamewekewa alama ya "X" yakisubiri utekelezwaji wa hukumu ya kuondolewa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam, je! mabango yaliyo katika mtindo huu kwenye nguzo za umeme mbona yamenyamaziwa?
Saturday, January 22, 2011
LIFT TAMU MWISHO WAKE NDIO MCHUNGU
Mfugo (Mbuzi) umekula lift hapo rahaa, tatizo huko mwisho wa safari ndio hatujui hatima yake ilikuwa nini. Au msomaji una habari safari iliishia vipi?
Friday, January 21, 2011
NOTI MPYA
Benki kuu ya Tanzania hivi karibuni imezindua noti mpya (pesa mpya) ambazo zimeanza kutumika sehemu mbali mbali nchini ila hata hivyo pamoja na jitihada za kuwaelimisha watu ujio wa noti mpya bado kuna watu wanazikataa pesa hizo kwa madai kuwa hawazitambui. Je kuna haja ya kutoa elimu tena kwa wananchi ama ziingie katika mzunguko wa pesa kidogo kidogo huku zikiendelea kupata upinzani toka kwa baadhi ya watu?
Sunday, January 16, 2011
BONGO KUMEKUCHA
Bongo Dar es salaam kuzuri, nani anabisha! Haya wadau wapi hapa? nipe jibu kama unapajua hapa. Picha hii ni moja ya sehemu ya jiji letu la Dar.
Saturday, January 15, 2011
DAR YAPENDEZA
Jiji la Dar es salaam nchini Tanzania siku za hivi karibuni limeanza kupendeza hasa katika maeneo ya fukwe za bahari, picha hii ni maeneo ya Msasani.
Sunday, January 9, 2011
AFRIKA KILA KITU KINAWEZEKANA
Askari wa kiafrika wakiwa wamepumzika na wakati huo huo wakitumia muda huo kunyoana nywele, cha kushangaza kwa asakari hawa ni kuwa mbali na silaha zao tena wakiwa katika vazi lisilo rasmi msituni, kweli Afrika kila kitu kinawezekana. Msomaji una maoni gani katika hili?
Monday, January 3, 2011
NI WAKATI WA KUAMKA SASA
Wasanii na wanamichezo wa Tanzania huu ndio wakati wa kuamka sasa kutumia nafasi zetu za kukubalika katika jamii kubuni njia nyingine ya kuongeza kipato zaidi ya sanaa, mfano mzuri tena wa kupongezwa ni wa msanii wa muziki Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jay Dee kwa kuamua kufanya muziki na biashara ikiwemo biashara ya maji ya kunywa yaliyozinduliwa mapema mwaka huu yenye jina lake na kisaniii. Hongera sana bint.
Sunday, January 2, 2011
WATANZANIA WAPO NYUMA YENU
Hawa ni kati ya viongozi wa kisiasa nchini Tanzania wenye ushawishi mkubwa toka kwa wafuasi wao, viongozi hawa ndio wamebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha amani inadumu kwa watanzania kutokana na kukubalika kwao na wafuasi wao. Je kama viongozi hawa wanakaa wanaongea kwa furaha kwa nini wafuasi wao wapambane mpaka wengine kupoteza maisha?
Friday, December 31, 2010
Wednesday, December 29, 2010
KWELI KIONGOZI HUYU NI FAMILIA YA MKULIMA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Mizengo Pinda a.k.a mtoto wa kulima, kweli ameonyesha yeye anatoka katika familia ya wakulima kwa kutumia muda wake wa mapumziko ya sikukuu ya x - mas na mwaka mpya kwa kujumuika na familia pamoja na wanakijiji katika kilimo, wakati viongozi wengine wanatumia mapumziko yao kama haya katika mahoteli ya kifahari ndani na nje ya nchi. Tanzania tunapenda kuona viongozi wa aina ya mheshimiwa Pinda.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















